TRUE STORY
Nilipanga kuifanya hii kuwa siri yangu lakini leo nimeona ni bora tena ni heri tu niiseme ili watu wajue kwani ni kazi rahisi kudanganya kabisa kuliko kufuuficha ukweli.
Wiki iliyopita, siku moja jioni, mida ya saa kumi na mbili na nusu niliondoka home (Mitaa ya Shekilango) nakuamua kufanya matembezi yangu ya jioni ambapo niliamua kwenda kwa miguu maeneo ya ubungo stendi ya mabasi ili nipoteze poteze muda then nilrudi zangu home kupumzika.
Nilipofika ubungo kama kawaida nikaona watu wengi huku kila mmoja akiwa na pilika zake za hapa na pale na kila mtu yuko na time zake, wengine na mabegi wengine biashara wengine vibaka na wengine ndio kama mimi. Nika ‘spend time’ mitaa hiyo mpaka mida ya saa mbili kasoro hivi nikaamua kurudi zangu home.
Wakati naanza kuondoka kurudi home ghafla nikasikia sauti ya mtu anayekuja nyuma yangu kama ananikimbilia huku akiniita bila kunitaja jina, nilipogeuka nikamuona binti mmoja mrembo mrebo ambaye kwa uhakika toka nimezaliwa sijawahi kumouna, kwa hiyo simfahamu kabisa.
Alipofika jirani yangu akavuta pumzi kwa pupa na kuitoa taratibu huku akiwa kimya hasemi chochote… na mimi nikaduwaa huku nikiwa namsubiri aseme nini anataka kuniambia….
Kaka samahani…!!
Bila samahani dada, tatizo nini mbona unahema sana ..!?
Naomba kuongea na wewe kaka, samahani kwa kukusumbua na kukupotezea muda wako mwenzio nina matatizo…!
Usijari dada, (huku tukiwa tunasogea pembeni kupisha wenye haraka zao wapite) niambie nini kinakutatiza, huenda kinatatulika dada…!!!
Kaka nimeangalia watu woote hapa nimeona wewe kidogo unaonekana ni mstaarabu na kwama unaweza ukanisaidia, nimeogopa sana nisije nikajielezea kwa kibaka akanifanyia kitu kibaya zaidi…!! Ila nilipokuona wewe nikamshukuru Mungu, nahisi wewe utanielewa kaka.
Sema basi nini tatizo dada we usijaari, me nimekuelewa.
Kaka, wewe ni mwenyeji hapa Dar?
Mh! Yes..! Kiasi..! Ndio, me ndio hapa nakaa (Huku nikijikanyaga kidogo)
Kaka, mimi nimetoka Mwanza, mimi ni mgeni kabisa hapa Dar, leo ndio siku yangu ya kwanza nafika, na huu usiku yani silewi lolote. Nimeibiwa kaka yangu, nimeibiwa pochi yangu ambayo ilikuwa na simu na pesa zangu zote…! Naomba nisaidie kaka yangu, ( Huku akianza tena kulia)
Dah! Pole sana dada yangu, kulia sana haitakusaidia. Sasa unataka me nikusaidiaje?
Vyovyote vile kaka.
Kwani ulikuwa unakuja Dar kwa nani? Nani mwenyeji wako? Wapi anakaa?
Anapokaa mimi sipajui, aliniambia mwananyamala sijui… mwenzio sielewi kaka me mgeni kabisa.
Ok! Nimekuelewa dada yangu, chukua simu yangu umpogie mwambie aje maeneo ya kuingilia mabasi halafu akubeep atatukuta hapa. Sawa? (Huku natoa simu yangu mfukoni)
Kaka, hata namba yake sijaikremu kichwani kaka yani ndio maana nimechanganyikiwa. Mara ya mwisho nimempigia nikiwa pale wanapaita Mbezi sijui, akasema anakuja kunichukua na gari, sasa nimeangalia stendi nzima sijamuona, huwa anaendesha Rav 4.
Daaaah….!! (Huku nahisi kucheka lakini najizuia) hapa dada huwezi kumpata mtu bila mwasiliano, Rav 4 ziko nyingi na kila baada ya dakika mbili zinapita nyingine.
Kwani huyo mtu kwako ni nani dada?
Boyfriend wangu. Na nyumbani nnimetoroka, wanajua niko chuoni.
Mbona unanipa wakati mgumu dada yangu, nitakusaidiaje?
Kaka naomba nifanyie usamaria mwema…. Nisaidie kaka yangu, huwezi kujua kwa nini Mungu kaniongoza nikuite wewe. Nisaidie…
Hebu twende…! (akabeba begi lake dogo la wastani mgongoni na lingine kushika mkononi na kuanza kunifuata) nikampeleka kwenye mgahawa jirani, nikamwambia agize chochote wakati tunafikiria nini tufanye. Akasema hajala kwa muda mrefu lakini hajisikii kula chochote zaidi ya soda. Basi nikaagiza soda mbili huku nikiendelea kuwaza nitamsaidiaje..!!
Huna ndugu yeyote hapa Dar? Nikamuuliza huku nikimkazia macho..
Ninaye, anakaa Masaki, ila namba yake ya simu pia sihifahamu. Sijui nina mkosi gani mimi jamani…
Anyway sio mkosi ndio maisha hayo…!! Me naitwa Alpha. Wewe unaitwa nani dada?
Me naitwa Sophia, naitwa Sophy. Nashukuru kukufahamu Alpha, ahsante kwa ukarimu wako, angekuwa mtu mwingine asingepoteza hata muda wake kunisikiliza, yaani bila wewe leo sijui ningefanyaje Alpha, nashukuru Mungu amenipa ujasijri wa kukukimilia na kukufuata…!
Sawa Sophy…! Sasa tunafanyaje? Unataka mimi nikusaidiaje?
Naomba unitafutie sehemu nilale, na nauli ya kwenda Arusha, kwani chuoni nakosoma ni Arusha.
Mh! Sophy, kusema kweli mimi hapa unaponiona hela sina, nilitembea tu na hiyo 10,000/= ili kulinda mfuko. Guest hapa Dar ni ghari sana , na nauli ya Arusha ndio daaah hii ishu sana aisee…!!
Alpha naomba nipelekwe hata kwenu, waambie wazazi wako ukweli. Watakuelewa tu!
Ah..! No mi sikai na wazazi…
Mh! Umeoa?
Hapana sijaoa..!!
Unakaa peke yako?
Ndio..!
Alpha, ni heri unipeleke hata kwako kuliko kuniacha hapa nikafanyiwa unyama. Wemwenyewe fikiria kaka yangu…
Ni kweli.. lakini hata mimi hunijui Sophy.
Lakini ni afadhali kwako kaka najiona niko salama, kuliko mateja wakinikuta sijielewi hivi watanifanyia kitu kibaya ambacho kamwe sitakisahau maishani mwangu, ni heri tu unipeleke kwako nitalala hata sebureni, hata chini. Lakini sio hapa, si sawa na kulala chini hapa stendi.
Sawa (Huku nikiwa na wasi wasi zaidi) sawa, basi agiza chakula kabisa ule kwani kwangu mimi sijapika. Akaagiza kiepe yai, nikaita bajaji, tukasepa.
Tulipofika home, nikamsaidia Begi lake moja tukaingia ndani. (Huku wote wawili tukiwa wenye mawazo mengi sana )
Tukala kiepe huku tukiongea mambo mengine, kama vile kazi, shule, na mambo mengine mengine, nikaanza kumuona anachangamka kidooogo.
Ilipofika mida ya saa nne na nusu hivi, nikaingia bafuni kuweka mambo sawa, kasha nikarudi nma kumwambia akaoge. Nikashangaa sana kuona akitoa nguo zake mbele yangu bila hata aibu, akajifunga taulo lake na kuingia bafuni kuoga. Akaniacha na mawazo mengi sana huki nikishika hiki na kuacha, mara kushika kile na kuacha…. Kama nimedata hivi… nikawaza huyu dada mbonaa… mbona..! sikupata majibu.
Alipo toka kuoga, akanitania kidogo… Zamu yako Alpha huku anasmail, anacheka. Nikajitupia taulo begani bila kumjibi chochote nikazama zangu bafuni. Huku nikiwa na wasi wasi nikafanya fast asana na kurudi ghafla kidogo. Alponiona alishtuka kama vile mtu aliyefumaniawa. Nilimkuta kashika ‘plasic bag’ ama mfuko wa mweusi nylon, umeandikwa SH. AMONS, aloponiona akaufunika ghafla na kuanza kuusokomeza kwa ndani ya begi kama vile anataka kuuficha. Hapo nikaanza kuweka doughts na huyu mdada mrembo, mweupe mweupe, ambaye ki ukweli ningemuacha pale ubungo stendi hakuna mtu amabaye angemuacha hivi hivi…
Nikaanza kutafuta style ya kumuingia ili nijui ni nini anaficha ndani ya begi lake ambalo wakati huo ndio alikuwa navuta zipu kulifunga kabisa.
Stella..!! kwanza kabisa, kabla sijasema lolote naomba ujisikie uko huru…!!
Me naitwa Sophy! Alpha kweli wewe ni msahaulifu sana .
Am sorry! Sophy naomba uniambie humo kweny mfuko umeficha nini? Na kwa nini unaficha? Unataka nikueleweje?
Nimekuficha nini Alpha?
Humo kwenye mfuko umeweka nini?
Haya ni mawe ya vito, nimeyaiba nyumbani kwa baba, nilikuwa namletea boyfriend wangu ili ayauze tupate hela.
Vito? Vito ndio nii? Sijakuelewa Sophy…!!
Hah! Hujui Vito? We wa wapi Alpha?
Niambie basi umeniacha njia panda, ujue nimesha anza kukuogopa wewe…!!!
Hizi ni dhahabu Alpha.
Dhahabu? Dhahabu hizi hizi dhahabu? (Nilihisi nachelewa kumlazimisha azitoe)
Ndio, ni dhahabu, (huku anafungua tena zipu na kuutoa ule mfuko) baba yangu ni mfanya biashara wa dhahabu, kama unaujua Mgodi wa dhahabu uliopo katika kijiji cha Nyaruyeye kata ya Nyarugusu wilaya ya Geita mkoani Mwanza. Huko ndio kwetu, me baba yangu ni tajiri sana , sema tu mimi na ulimbukeni wangu wa mapenzi ndio najikuta naangukia kwenye mikasa kama hii, nimeibiwa laki nane pale stendi, blackberry tourch na cheni zangu za dhahabu sita, nilikua namletea honey wangu Devid. Wamechukua wahuni wasiokuwa na utu wala huruma hata chembe. (Akamaliza)
Hebu nioneshe…. Nitoe ushamba basi…! Akatoa ule mfuko, kwa macho yangu nikaona dhahabu nyingi vile kwa mara ya kwanza katika maisha yangu.
Hii inaweza hata kufika kilo moja na nusu Alpha, huko home lazima baba kichwa kimuume, lakini ni lazima atajua tu nimimi ndio niliyechukua, maana hii sio mara yangu ya kwanza kumuibia.
Mh! Sasa hii yote inathamani gain? (Nikamuuliza kwa tama)
Hii dhahabu nyingi sana , hata hiyo kilo moja nanusu nimekadilia tu, inadhamani kubwa sana hii.. hapa mtu anajenga nyumba hapa. Shauri zako.
Mh!
Unaguna nini Alpha…?
Sasa si twende mjini tukauze hizo kesho kwa masonara halafu upate hiyo nauli ya Arusha?
Nauli haitakuwa tatizo Alpha, nashukuru nimepata pa kulala… nashukuru pia umenipokea vizuri, mambo mengine yatakaa sawa tu usijaari.
(Moyo wangu ukaanza kunituma ujinga, nusu unaniambia niibe begi nisepe nimwachie geto, nusu unaniambia nibaki ila nifanye juu chini hata kwa kumdanganya danganya ili aniachie dhahabu)
Mida ya saa tano na nusu ilipowadia, nikamwambia sasa inakuwaje?
Kuhusu nini?
Me nataka kulala Sophy.!! najihisi kuchoka sana .
Hata mimi nimechoka Alpha, tulale basi…!!
(Huku nikiwaza jinsi ya kulala) Ulisema.. uta….!!
No! Alpha, silali chini mimi, naomba tulale tu wote bwana, kila mtu anajieshimu, tulale tu kwanza mimi kulala chini sijawhi… kwani wewe unawasiwasi?
No!
Sasa kwanini Sophy alale chini? Hahahahaha, (Anacheka)
Kwa hiyo tunalala wote? Nikamuuliza kwa msisitizo zaidi
Of course! Hata mzungu wa nne poa. Ila sio chini.
Haya basi, me nazima taa… (Nikampima kidogo)
Ah! No usizime kwanza, iache nitaizima mwenyewe…we panda kitandani ulale “Akanijibu huku akijiamini sana ”
(Nikaficha kwanza funguo ili asije akanitoroka au kuniibia)
Me nikapanda kitandani nikavuta shuka nusu nikazuga kama nimelala (Huku nikiwaza dhahabu)
Akatoa taulo lake kiunoni , akavaa nguo yake ya kulalia, akazima taa, kasha akapanda kitandani. Upande ule ule niliogeukia mimi.
Akanisogelea jirani kabisa huku miili yetu imegusana.
Alpha unafanya kazi gain?
Aaah! Nipo tu, si unajua mjini..!!! Kujishikiza shikiza tu….!!
Ila nimekupenda jinsi ulivyo mpore na mkarimu, mtu mwingine asingenielewa, sio rahisi kabisa. Leo ningepoteza kila kitu nilicho nacho. Nataka nikupe zawadi…
Zawadi gain (hapo akili yangu ishadata zamani sana , sielewi A wala B)
Nitakupa nusu ya hizo dhahabu ukauze, halafu nikirudi home nitamwambia Dad akutafutie kazi nzuri pale Migodini… ili mradi tu umesoma we usiwe na wasi wasi. Utaenjoy!! Devi tatizo lake hajasoma , hata ile Rav 4 tuliiba madini ya baba. Ila ananiboa hataki kujiendeleza, anazinguliwa na vi hela hela vya baba yangu ambavyo ni mpaka mimi niibe au nimgawie zangu, hataki nay eye kujituma na kujenga maisha yake, haelewi kuwa hivi vitu huwa vinaisha, hela zenyewe za madini, kesho na kesho kutwa utashangaa zimekatika utadhani zinamajini. Kila siku akija mwanza au akinifuata chuo Arusha namwambia aanzishe biashara hataki, shauri zake.
Kwani huyo Devy ana umri gain? (Nilimuuliza huku natetemeka)
He is veru Old, kanizidi sana hata kukwambia naona aibu, I am nont deserving him basi tu…. Ila Alpha nakupenda sana wewe sio siri, you are so cute. (una baby face) Can’t you be my honey?
Akazidi kunisogelea zaidi…! Akanigeukia na kunikumbatia kabisa…
Nikaona isiwe ishu, nikarespond, loadin…
Ile kuamka asubuhi, nikajikuta niko peke yangu kitandani. Moyo ukapiga paa……!!!!
Nikakurupuka kitandani ghafla. Sikuona nguo ya Sophy hata moja, wala mabegi yake…. Kucheki mlango nikaona bado umefungwa, kuangalia mahali nilipoficha funguo nikaikuta ipo, tena ipo vile vile kama ambavyo niliiweka. Moyo ulizidi kushtuka na kuanza kunidunda kwa kasi zaidi, nikaingia bafuni, sikuona dalili yoyote ile hata kama kuna mtu aliingia toka nilivyotoka kuingia mimi jana usiku.
Ghafla nikaanza kutetemeka mwili na jasho jembamba likaanza kunitoka, nilitamani kupiga makelele ili nipate msaada wa majirani, lakini nikajikaza kiume na kuendelea kutafakari kwa kina kilicho nitokea, nikafungua mlango. Nikatoka nje, nikaona kila mtu yoko na pilika zake watu hata hawana habari na mimi… nikarudi ndani, nikashika simu yangu, kucheki saa, ilikuwa mida ya saa nne asubuhi… Nilikuwa nahisi njaa kali kama vile mtu ambaye hajawahi kula aina yoyote ya chakula kwa muda mrefu sana . Nikiwa nimekaa mkao wa kukata tama, nikaona sahani iliyokuwa inamabai ya ndizi na nyama chini ya meza yangu ya chakula, nikakumbuka chakula hicho nilikula jana mida ya saa moja na nusu nikiwa najiandaa kulala. Ghafla fahamu ikanirudia. Khaaaaa!!!!
“KUMBE NILIKUWA NAOTA”
Kumbe Habari za Sophy ni ndoto tu, Mungu wangu, nikaanza kurukaruka huku nikimshukuru mungu nakusema kwa nguvu, “Nashukuru Mungu kumbe ni ndoto”
***
Niko na maandalizi ya kuanza kuandika RESEARCH, nilikuwa nafanya tu mazoezi ya KEYBOARD na kuangalia SPEED na ACCURACY. Sorry for taking your time to read this annoying story.
Alpha Amos Ambokile.
0717 312028
0767 283131